Katibu Mkuu mpya wa NATO afanya ziara ya kwanza Ukraine
3 Oktoba 2024Mkuu mpya wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Mark Rutte ameitembea Ukraine katika ziara yake ya kwanza akiwa katiika nafasi hiyo na kumpongzea rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwamba mpango wa ushindi katika vita vyake dhidi ya Urusi.
Akizungumza nchini Ukraine, Katibu mkuu mpya wa NATO alimwambia haya rais wa Ukraine.
Soma pia: Rutte: "Sina hofu na utawala ujao wa Marekani"
"Nimekuja Ukraine mwanzo wa kutimiza jukumu langu kama katibu mkuu, kukueleza waziwazi wewe, watu wa Ukraine na kila mtu kwamba NATO inasimama na Ukraine.
Kama Katibu Mkuu mpya wa NATO, ni kipaumbele changu na fursa kwangu kuuendeleza uungaji mkono huu kwa Ukraine. kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha Ukraine inashinda,"
Kwa upande wake rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Zelenskiy aliuambia mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari kwamba angependa
kuona washirika wake wakiwasaidia zaidi katika kupambana na makombora na droni za Urusi zilizotengenezwa nchini Iran.