Makala ya Karibuni wiki hii inazungumza na mwanamitindo mkongwe kutoka nchini Tanzania, Diana Magesa. Diana ni mwanamitindo mbunifu wa mavazi na vitu vya urembo vya kike.Lakini ubunifu wake ni wa aina ya pekee kabisa wa kutumia maarifa makubwa sana nje ya mipaka ya kawaida. Saumu Mwasimba ndiyo nahodha wako.