SiasaUfaransa
Karibu wagombea 200 wa bunge nchini Ufaransa wajiengua
2 Julai 2024Matangazo
Takwimu hizi zimetolewa na shirika la habari la Ufaransa, AFP.
Muungano wa vyama vya mrengo wa kushoto wa Rais Emmanuel Macron unajaribu kukizuia chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha National Rally kuchukua madaraka.
Mahasimu hao wa kisiasa wanatumai kwamba kujiondoa huko kwa kimkakati kuelekea duru ya pili ya uchaguzi itakayofanyika Jumapili ijayo, kutakizuwia chama cha National Rally kinachoongozwa na Marine Le Pen kupata wingi wa kutosha wa viti 289 kati ya jumla ya viti 577 katika bunge la taifa.
Chama hicho kilishinda duru ya kwanza ya uchaguzi huo iliyofanyika Jumapili iliyopita kwa kupata zaidi ya kura milioni 10.6 na kuibua hofu kwamba huenda kikachukuwa madaraka kwa mara ya kwanza katika historia ya Ufaransa.