Karibu 2024, kwaheri 2023
1 Januari 2024Mwaka 2024 unakaribishwa wakati watu wengi wakitarajia nyakati bora licha ya mizozo katika maeneo ya Mashariki ya Kati, Ukraine na kwengineko barani Afrika.
Eneo la Kanda ya Pasifiki ndiyo limekuwa ka kwanza kuingia katika mwaka wa 2024.
Tokyo na Seoul maadhimisho yamefanyika kwa kumefyatuliwa fashifashi.
Sehemu za Mashariki ya Mbali zimeukaribisha 2024 kwa maonyesho makubwa ya fashifashi, ikijumuisha Seoul na Tokyo.
Huko Japan, kengele za hekalu zililia kote nchini wakati watu wengi walipokusanyika kwenye mahekalu makubwa na madogo ya ibada kwa lengo la kukaribisha mwaka mpya.
Katika Hekalu la Tsukiji huko Tokyo, wageni walipewa maziwa ya moto na supu iliyopikwa kwa mahindi bila malipo walipokuwa wamesimama kwenye foleni ili kupiga kengele kubwa kabla ya kuagwa mwaka 2023.
Sharamrashamra za mwaka mpya kwa Australia
Jiji kubwa zaidi la Australia, Sydney, ambalo limejitangaza kuwa "Mji mkuu wa Mwaka Mpya wa ulimwengu," limeangaziwa kwa kina kwa maonyesho yake ya kitamaduni ya fashifashi juu ya daraja kubwa kwenye eneo la bandari lijulikanalo kama "Harbour Bridge."
Kulikuwa na giza katika daraja hilo kwa dakika chache kabla ya kuanza kuhesabu kwa kutoa nafasi kwa onyesho la kupendeza la rangi zinazong'aa baada ya saa sita usiku.
Maonyesho hayo, yaliyohusisha takriban tani 8 za fataki, yalishuhudiwa na maelfu ya watu waliokusanyika kwenye maeneo ya mbele, kandoni mwa bahari.
Kisiwa cha Kiribati miongoni mwa maeneo ya mwanzo kuadhimisha mwaka 2024
Kiribati kama sehemu ya visiwa vya Line ni miongoni mwa maeneo ya mwanzo ya ulimwengu kukaribisha mwaka wa 2024, ingawa hakukukuwa na matukio makubwa ya maadhimisho yaliyopangwa katika kisiwa kikuu cha eneo hilo cha Kiritimati.
Soma zaidi:Polisi wa Ujerumani waimarisha ulinzi katika Kanisa Kuu la Cologne kufuatia kitisho
Wakazi wa visiwa hivyo huwa na tabia ya kusherehekea mabadiliko ya mwaka kwa kula nyama ya nguruwe ya kuchoma, samaki aina ya kamba na vyakula vingine vya kitamaduni, vikiambatishwa na kinywaji maarufu maji ya madafu.
Chanzo: DW