1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz anapanga kuzungumza na rais wa Urusi Vladimir Putin

10 Juni 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema kuwa anapanga kuzungumza na rais wa Urusi Vladimir Putin kwa njia ya simu kumuhimiza kuviondoa vikosi vya Urusi nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4SQMD
Deutschland | Olaf Scholz am Evangelischen Kirchentag
Picha: Thomas Lohnes/epd-bild/picture alliance

Akihutubia kongamano la kanisa la Kiprotestanti la Ujerumani mjini Nuremberg, Scholz amesema aliwahi kuzungumza na Putin kwa njia ya simu katika siku za nyuma na kwamba anapanga kufanya hivyo tena. Scholz ameongeza kuwa sio busara kuilazimisha Ukraine kuidhinisha na kukubali uvamizi huo wa Urusi na kwamba baadhi ya maeneo yake yageuka ghafla kuwa ya Urusi.

Scholz asema atajitahidi kuona NATO haijumuishwa katika vita

Kansela huyo pia amesema atajitahidi kuona kwamba jumuiya ya kujihami ya NATO haijumuishwi katika vita hivyo. Urusi na Ukraine zote zimeripoti mapigano makali nchini Ukraine hapo jana Ijumaa lakini bado haijabainika wazi iwapo mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Ukraine yaliosubiriwa kwa muda  mrefu bado yatafanyika.