Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz aanza ziara barani Afrika
4 Mei 2023Matangazo
Ziara ya Scholz hiyo italenga juhudi za utatuzi wa migogoro na ulinzi wa amani, tabia nchi, mada kuhusu nishati jadidifu pamoja na madhara ya vita vya Urusi nchini Ukraine.
Scholz anatarajiwa kwanza kutua Ethiopia kwa mazungumzo na serikali ya taifa hilo pamoja na maafisa wa Umoja wa Afrika.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka miwili katika jimbo la Tigray vilisababisha vifo vya mamia ya maelfu ya watu.
Baadaye jioni, Scholz ataelekea Kenya, nchi ambayo ni mshirika muhimu zaidi kwa Ujerumani katika kanda ya Afrika Mashariki.
Kenya imekuwa ikiongoza jukumu muhimu la upatanishi na usuluhishi wa mizozo ya kikanda na tayari imejitolea kushiriki katika juhudi za kupunguza machafuko ya Sudan.