Kansela Scholz asema muungano wa Ujerumani umekamilika
3 Oktoba 2024Matangazo
Scholz amesema hayo kwenye maadhimisho ya miaka 34 ya muungano wa Ujerumani yaliyofanyika Schwerin ambao ni mji mkuu wa jimbo la Mecklenburg-Vorpommern la kaskazini mashariki mwa Ujerumani.
Kiongozi huyo ameeleza kwamba kulinganisha na hali ya mwaka 1990 hatua kubwa imepigwa.
Soma pia: Ujerumani inaadhimisha miaka 34 ya muungano
Kuhusu hali ya kisiasa nchini, Kansela wa Ujerumani amesema anatarajia kuwepo changamoto kutokana na makundi yenye siasa kali za mrengo wa kulia.
Ameeleza kwamba siasa za aina hiyo zitaiathiri Ujerumani, Uchumi wake na hadhi yake duniani. Hata hivyo amesisitiza kwamba idadi kubwa ya Wajerumani wanaunga mkono misingi ya demokrasia.