Kansela Scholz atetea mipango ya pensheni katika bajeti 2025
12 Septemba 2024Katika mjadala uliofanyika bungeni jana, Kansela Scholz alisema kwamba serikali yake ina mipango mikubwa kuhusu uhakika wa viwango vya pensheni.
Kwa upande wake kiongozi wa upinzani wa chama cha mrengo wa wastani kulia cha CDU, Friedrich Merz ameishambulia bajeti hiyo na kuituhumu serikali ya Scholz kwa kuharibu soko huria.
Soma pia:Ujerumani yasema bajeti finyu haitawazuia kuisaidia Ukraine
Merz amedai kuwa muungano wa Scholz umeifanya sera ya kijamii kuwa mzigo kwa kizazi kichanga ambacho kitalazimika kulipa mafao zaidi.
Kiongozi huyo wa upinzani amesema kila uamuzi unaofanywa na serikali ya Kansela Scholz umezidisha hali ya ushindani kwa uchumi wa Ujerumani. Scholz ametoa utetezi huo wakati waziri wake wa ulinzi akikabiliwa na maswali magumu juu ya ufadhili wa jeshi.