Kansela Scholz akutana na Rais Erdogan
15 Machi 2022Akizungumza katika mkutano wa pamoja na Rais Recep Erdogan, Kansela Olaf Scholz akiwa katika ziara yake ya kwanza Uturuki tangu aingie madarakani alisema kama washirika wa Jumuiya ya NATO wameziweka wazi fikra zao za pamoja na wasiwasi.
Erdogan kadhalika aligusia uhusiano wake na Urusi, amboa uliufanikisha kwa taifa lake kuwa mwenyeji wa mkutano wa kwanza kidemokrasia wa juma lililopita ambao uliowajumisha mawaziri wa mambo ya nje wa Urusi na Ukraine.
Alisema lazima wawalinde marafiki zao kwa pamoja Zelenskiy na Putin. Tofauti na mataifa ya Ulaya Uturuki haijafunga anga yake kwa ndege za Urusi lakini Erdogan anasema taifa lake limefanya kila lililomuhimu katika kutekeleza kanuni za Umoja wa Mataifa.
Mazungumzo ya amani ya Ukraine yanaendelea Jumanne.
Rais wa Ukrayine Volodymyr Zelenskiy amesema mazungumzo ya amani kati ya na Urusi yataendelea leo Jumanne. Kiongozi huyo pia amesema amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Naftali Bennett ikiwa kama sehemu ya jitihada ya kumaliza vita.
Ulaya yapitisha vikwazo vipya dhidi ya Urusi.
katika hatua nyingine Umoja wa Ulaya Jumatatu ulipitisha vikwazo vipya dhidi ya Urusi kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine, huku wanadiplomasia wakisema Roman Abramovich ni miongoni mwa watu walio orodheshwa.
Uenyekiti wa umoja huo ambao kwa sasa unashikiliwa na Ufaransa, umeandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba mabalozi wa mataifa 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya wameridhia ngwe ya nne ya kitita cha vikwazo, kikiwagusa watu binafsi na makampuni, yenye kuhusishwa na mashambulizi ya Ukraine.
Wanadiploamisa watatu waliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP, bilionea na mmiliki wa klabu ya soka ya Chelsea, Abramovich ameongezwa katika orodha ya matajiri wa Kirusi ambao mali zao katika Umoja wa Ulaya ni pamoja na majumba makubwa ya kifahari.
Uhusiano wa tajiri Abramovich na Rais Putin wamweka matatani.
Hatua hiyo ya Abramovich inafuatia ile ya Uingereza na Canada, ambazo zilimwekea tajiri huo katika orodha za vikweazo vyao. Kwa mujibu wa wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya sababu zinazoelezwa ni kutokana na mfanyabiashara huyo kuwa na ushawishi nchini Urusi na uhusiano wa karibu na raisVladimir Putin.
Kwa mujibu wa jarida la Forbes Abramovich, mwenye umri wa miaka 55, anautajiri wa dola bilioni 12.4 .
Ijumaa iliyopita Ijumaa iliyopita Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen katika ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya nchini Ufaransa, alitangaza duru ya hivi punde zaidi ya vikwazo vilivyokubaliwa na mataifa washirika kwamba vitaitaitenga zaidi Urusi na kupoteza rasilimali inazozitumia kufadhili vita hivyo alivyoviita kuwa ni vya kinyama.
Vyanzo: AFP/RTR