1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Olaf Scholz atoa zingatio Ulaya katika ziara yake ya kwanza

11 Desemba 2021

Kansela mpya wa Ujerumani Olaf Scholz, ametumia ziara yake ya kwanza Ufaransa na Ubelgiji kusisitiza hamasa ya serikali yake katika kushirikiana kwa hali ya udharura katika masuala ambayo Umoja wa Ulaya inakabliana nayo.

https://p.dw.com/p/447a3
Frankreich Paris | Emmanuel Macron empfängt Bundeskanzler Olaf Scholz
Picha: Eliot Blondet/abaca/picture alliance

Akizungumza katika mkutano wake wa pomoja na Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, Scholz alisema ni muhimu Ulaya ikasimama pamoja na kushirikiana kwa ukaribu.

Nae Von der Leyen aliikaribisha fursa ya kufanya kazi pamoja na Scholz, baada ya kushirikiana huko nyuma katika serikali ya muungano ya mtangulizi wake, Angela Merkel. Scholz kwa sasa anaongoza muungano wa pande tatu wa chama chama chake cha Social Democrats (SPD), lakini wakati akiwa waziri wa fedha katika baraza la mawaziri la Merkel alikuwa ni mtu mwenye kufahamika sana mjini Brussels.

Kansela mpya wa Ujerumani na changamoto nyingi zinazomkalibili

Belgien Olaf Schol und Ursula von der Leyen in Brüssel
Kansela Olaf Scholz na Ursula von der Leyen Picha: Johanna Geron/REUTERS

Kumekuwepo na mkururo wa changamoto ambazo zinamsubiri kiongozi huyo katika kipindi hiki cha mwanzo kabisa cha muhula wake, zikiwemo za mvutano mkali wa Urusi, unaogubikwa na hofu ya serikali ya taifa hilo kuweza kupanga uvamizi mwingine katika ardhi ya Ukraine.

Kwa pamoja Sholz na von der Layen wameionya onyo Urusi, kwa kuieleza kitendo chake cha kuwakusanya wanajeshi katika eneo la mpaka wake na Ukraine si jambo linalokubalika. Wakati Leyen akisisitiuza kwamba uchokozi wowote una ghamara zake.Scholz anasema jukumu lililopo kwa sasa ni kuizuia serikali ya Moscow kufanya ukiukwaji wowote wa kimipaka.

Mataifa lazima yasaidiwe katika kukabiliana na mdodoro wa kiuchumi

Kansela mpya wa Ujerumani vilevile amepata fursa ya kujadiliana na afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya kuhusu janga la Covid-19, sambamba na mataifa wanachama wa umoja huo, mjadala uliojikita katika namna gani ya wanawza kuujengea uwezo uchumi ulionyong'onyea. Amesema wanataka kuyasaida mataifa yote ili kuinua hali za chumi zake.

Mapema Ijumaa, Kansema wa Ujerumani alitoa hakikisho la taifa lake kuwa na ushirikiano na Ufaransa, katika mkutano na mwenyeji wake Rais Emmanuel Macron. Hii nayo ni ziara ya kwanza ya kuwasili kwake mjini Paris tangu achukue hatamu ya uongozi Jumtano iliyopita.

Akizunguma katika kasri la Elysee,Scholzanameeleza kwa namna gani ambavyo Ulaya inaweza kujengewa umadhubuti, uhuru wa kimipaka katika maeneo yote. Na mwenyeji wake Macron alijibu kwa ahadi ya kufanya kazi kwa ushirikiano akisema hali hiyo itaendelea kama ilivyokuwa kwa Kansela aliyepita Angela Merkel. Viongozi hao wawili walijadiliana kuhusu ushirikiano katika mabadiliko ya tabia nchi, ujenzi wa miundombinu ya kidijitali na uhamiaji.

Chanzo: DPA