Uchumi
Kansela Olaf Scholz azungumza na rais wa Kazakhstan
16 Septemba 2024Matangazo
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz yuko ziarani nchini Kazakhstan, ambako amekutana mjini Astana leo na rais Kassym-Jomart Tokayev kuhusu masuala ya ushirikiano wa kiuchumi.
Kansela Scholz ambaye Kazakhstan ni kituo cha pili cha ziara yake ya siku tatu katika eneo hilo la Asia ya Kati, aliyoianzia, Uzbekistan, amesema atafanya kila awezalo kuimarisha uwezekano wa kuwepo mahusiano mazuri ya kiuchumi huku akitowa mwito kwa kuendelea ushirikiano katika sekta ya mali ghafi.
Kazakhstan ni nchi ya tatu msambazaji wa mafuta kwa Ujerumani baada ya Norway na Marekani. Takriban asilimia 11.7 ya petroli ya Ujerumani inatokea katika nchi hiyo yenye nguvu katika kanda ya Asia ya Kati.