Kansela Olaf Scholz ahimiza kuachana na nishati ya mafuta
2 Desemba 2023Matangazo
Amewaambia wajumbe kutoka katika pande zote za ulimwengu kuwa lazima kuwepo na dhamira thabiti katika kutekeleza lengo hilo. Na kuongeza kuwa wote kwa pamoja wanaweza kuanzisha jitihada ya utekelezaji katika mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi.Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa Ujerumani, bado upo uwezekano wa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu inayoharibu mazingira katika muongo huu kwa chini ya kiwango cha nyuzi joto 1.5 katika viwango vya celsius kwa zingatio la mkataba wa Paris wa mwaka 2015.Kansela Scholzamesema sayansi inasema wazi kuwa jitihada hizo zinapaswa kuharakishwa, pamoja na kuwepo na mivutano ya kimataifa, akimaanisha vita katika Ukanda wa Gaza na Ukraine, ambayo pia ni mada kuu kwenye mkutano huo.