1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Kampuni za Ujerumani kuwekeza zaidi barani Afrika mwaka 2023

28 Desemba 2022

Makampuni ya Ujerumani yanataka kuimarisha zaidi shughuli zake mwaka unaokuja pamoja na kuongeza kwa asilimia 43 uwekezaji barani Afrika hasa katika sekta ya nishati za haidrojeni na gesi iliyosindikwa.

https://p.dw.com/p/4LU8w
VW Logo Symbolbild
Picha: AP

Hayo ni kulingana uchunguzi ambao shirika la habari la Reuters limeona nakala yake hapo jana.

Kulingana na takwimu za wizara ya uchumi, makampuni ya Ujerumani yaliwekeza takriban euro bilioni 1.6 barani Afrika mnamo mwaka 2021, ambapo takriban euro bilioni 1.1 zilielekezwa katika nchi za Afrika zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara.

Mkuu wa chama cha biashara kati ya Afrika na Ujerumani Christoph Kannegiesser amesema wakati taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya likilenga kupunguza utegemezi wake kwa gesi ya Urusi tangu ilipoivamia Ukraine, wanaona fursa kubwa katika sekta ya nishati barani Afrika.