Kampuni mafuta Libya kufungua shughuli za bandari
26 Oktoba 2020Matangazo
Siku ya Ijumaa kampuni hiyo ilisema inatarajia uzalishaji wake wa mafuta utafikia mapipa 800,000 kwa siku katika kipindi cha wiki mbili na kuongezeka hadi mapipa milioni 1 katika muda wa wiki nne zinazokuja baada ya kufungua tena shughuli za kawaida kwenye bandari za Ras Lanuf na Es Sider.
Kampuni hiyo imekuwa ikiondoa kwa awamu vizuizi vya uzalishaji mafuta hasa kwenye maeneo ambayo hakuna tena mapigano kati ya pande hasimu nchini Libya.
Marufuku ya kuzalisha na kusafirisha mafuta iliwekwa mwezi Januari na vikosi vya mbabe wa kivita Khalifa Haftar na ilifikia mwisho mwezi Septemba baada ya mazungumzo kati ya Jenerali huyo na serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa.