Afrika Kusini kuanza kutengeneza pete za ukeni za kuzuia VVU
30 Novemba 2023Matangazo
Kampuni ya afya ya Kiara iliyopo mjini Johannesburg itaanza kutengeneza vifaa hivyo katika miaka ijayo na inakadiria kutengeneza hadi kinga milioni 1 kwa mwaka.
Hadi sasa kinga hiyo iliyotengenezwa mfano wa pete, karibu 500 zinapatikana kwa sasa kote barani Afrika na hutolewa bure kwa wanawake.
Aina hiyo ya kinga inayowekwa sehemu ya siri ya mwanamke, husambaza dawa inayozuia maambukizi ya VVU na tayari zimeidhinishwa na Shirika la Afya Duniani WHO na katika nchi karibu kumi na mbili.
Kulingana na takwimu ya WHO, Virusi vya Ukimwi bado ni sababu kuu ya vifo kwa wanawake barani Afrika na asilimia 60 ya maambukizi mapya hutookea kwa wanawake.