1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni ya kubadili majina ya enzi za ukoloni nchini Uganda

Saleh Mwanamilongo
19 Juni 2020

Kampeni inaendelea nchini Uganda ya kubadili majina na kuzing'oa sanamu za viongozi waliohusika na ukatili wa kikoloni.Barabara nyingi mjini Kampala zimepewa majina ya Wakoloni wa zamani wa Uingereza.

https://p.dw.com/p/3e1wf
Sanamu ya Captain John Fane Charles Hamilton ikiondolewa kwenye Uwanja wa Hamilton, nchini Uingereza.
Sanamu ya Captain John Fane Charles Hamilton ikiondolewa kwenye Uwanja wa Hamilton, nchini Uingereza.Picha: Getty Images/AFP/M. Bradley

Kuna kampeni inayoendelea nchini Uganda ya kubadili majina na kuzing'oa sanamu za viongozi waliohusika na ukatili wa kikoloni. Kundi la vijana wanaondesha kampeni hiyo nchini Uganda,wanategemea kufikia malengo yao kabla ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki kuadhimisha tarehe 9 oktoba,miaka 58 ya uhuru wake kutoka kwa Uingereza.

Hiyo ni barabara Speke, kwa jina la John Hanning Speke,mzungu wa kwanza kuuona mto Nile.Barabara nyingi mjini Kampala hasa zile za pembezoni mwa mji zimepewa majina ya Wakoloni wa zamani wa Uingereza.

Sir Hillary Johnston,Henry Edward Clovile,King's Africa Rifle,Princess Ann, Mwanamfalme Charles,Malkia Elisabeth wote walipewa majina kwenye barabara za kampala.

Katika wimbi la maandamano lililofuatia kuuawa kikatili kwa Mmarekani mweusi Goerge Floyd mjini Minneapolis,Marekani,baadhi ya watu wamehisi kwamba ni wakati  sasa kwa Waafrika kuwaenzi mashujaa wao.

Profesa kakule, muhadhiri kwenye chuo kikuu cha Makerere, ndiye anaendesha kampeni hiyo.Anasema nyakati zimebadilika na raia wa Uganda hawajaridhishwa na vitendo walivyofanya wakati wa enzi za ukoloni.

''Nimetoa mfano wa kanali Colville,alikuwa kamanda aliyeendesha vita dhidi ya Banyoro na akaunganisha eneo hilo kwenye nchi ya Uganda.Kwa mtizamo wangu ni kwamba  majina hayo yanaweza kutolewa kwa watu waliochangia kwa ajili ya mabadiliko mazuri kwa nchi''.

Senegal Französischer Offizier mit Kolonialsoldat
Picha: picture-alliance/AP Images

Mwengine anayechangia kwenye kampeni hiyo ni Mwanahistoria Apollo Mukubaya.Anasema kuna Waganda wengi ambao wanatakiwa kuenziwa kwa kupewa majina yao kwenye barabara au mikoa.

''Ufahamu kwamba wote hawa ni wanajeshi.Inaoneysha kwa njia nyingi kwamba eneo hili lilidhibitiwa  na wanajeshi kwa sababu hawa walikuwa ni makanali waliosherehekewa baada ya kuzitimua taasisi walizo zikuta hapa''.

Wanaoendesha kampeni hiyo ya kubadili majina ya wakoloni wanalenga kuitisha maandamano ili kuomba wawakilishi wao kwenye baraza la wawakilishi la mji wa Kampala  kupitisha sheria inayobatilisha majina yote ya kikoloni.

Meya wa mji wa Kampala Elias Lukwago, amekubaliana na kampeni hiyo lakini amesema kwamba hatua hiyo itachukuwa muda. Anasema hakuna sababu hata moja ya kuwaenzi madikteta ambao walikanyaga haki yetu na kushiriki katika biashara vya watumwa.

Lakini kwa upande wake mwanasheria mjini Kampala, Bernard Olok anasema hakubaliani na wazo hilo,akielezea kwamba historia haiwezi kufutwa.