1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Kampeni ya nchanjo kuzinduliwa Gaza licha ya mashambulizi

Angela Mdungu
31 Agosti 2024

Wakati shirika la Afya duniani WHO na washirika wake wakitarajiwa kuanzisha kampeni ya chanjo ya watoto dhidi ya Polio huko Gaza, maafisa wa Palestina wamesema Israel imewauwa watu wanne.

https://p.dw.com/p/4k875
WHO na washirika wake kuanzisha kampeni ya chanjo ya watoto dhidi ya Polio huko Gaza
WHO na washirika wake kuanzisha kampeni ya chanjo ya watoto dhidi ya Polio huko GazaPicha: Omar Ashtawy/APA Images/Zumapress/picture alliance

Vifaa hivyo vilipaswa kupelekwa katika hospitali ya Emirati ya Gaza. Hata hiyvo jeshi la Israel limesema wanaume hao walikuwa wamebeba silaha huku maafisa wa Palestina wakidai kuwa walikuwa ni wafanyakazi wa kampuni ya usafirishaji katika ukanda huo.

Hayo yakiendelea, jeshi la Israel limesema Wapalestina wawili wameuwawa usiku wa kuamkia Jumamosi (31.08.2024) wakati walipokuwa wakijiandaa kufanya mashambulizi ya mabomu katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu ambapo Israel inaendesha operesheni ya kijeshi kwa siku ya nne.

Awali jeshi la Israel liliripoti mlipuko uliotokea katika kituo cha mafuta katika eneo la makazi ya walowezi la Gush Etzion. Jeshi lilisema kuwa shambulio hilo lilikuwa jaribio la kulipua gari lililofanywa na magaidi. Katika shambulio hilo mwanajeshi mmoja na mwingine wa akiba walijeruhiwa.