KAMPALA:Msaada wa chakula waanza kuingizwa na WFP
17 Oktoba 2007Matangazo
Shirika la Chakula Duniani WFP limeanza shughuli ya kuangusha magunia ya chakula kwa helikopta nchini Uganda tangu mafuriko kuanza.Mafuriko hayo ni mabaya zaidi kutokea katika kipindi cha miaka 35.
Katika taarifa iliyotolewa hapo jana operesheni hiyo ni juhudi za mwisho za kujaribu kutoa msaada kwa maelfu ya watu wanaokabiliwa na athari za mafuriko baada ya barabara muhimu kusombwa na maji.
Uganda ni moja ya mataifa yaliyoathiriwa na mvua kubwa na mafuriko yaliyoenea katika eneo la afrika mashariki na magharibi katika kipindi cha miezi michache.Mafuriko hayo yamesomba vijiji,kuharibu mazao pamoja na kusababisha vifo vya mifugo.