KAMPALA.Kiongozi sugu wa LRA adaiwa kuwawa Kaskazini mwa Uganda
24 Juni 2005Matangazo
Wanajeshi wa Uganda wamedai kumuua kiongozi sugu wa kundi la waasi wa LRA baada ya kumvamia mafichoni mwake katika eneo la Kaskazini wilayani Gulu.
Msemaji wa jeshi kanali Bantariza amesema wanajeshi hao wamemuua Opiro Anaka pamoja na mkewe. Na walinzi wake wawili Walipokuwa wakijaribu kukimbia .
Msemaji huyo wa jeshi amesema waasi waliopo chini ya uongozi wa Opiri wamekuwa wakifanya mashambulizi mara kwa mara katika vijiji vya wilaya ya Gulu na wamehusika katika uvamizi mbya zaidi mnamo mwezi uliopita kwenye kambi ya wakimbizi na kuwauwa watu sio chini ya 16.