Kamerhe aunda muungano mpya wa kisiasa
24 Januari 2024Matangazo
Muungano huo mpya umeundwa ndani ya ule wa Union Sacrée unaovijumuisha vyama washirika wa Rais Felix Tshisekedi.
Kuundwa kwa PCR kumeibua wasiwasi wa uwezekano wa kuyumba mshikamano miongoni mwa vyama vinavyoshirikiana na Rais Tshisekedi katika kuiongoza Kongo.
Makundi manne ya kisiasa yanayounda muungano huo yanawajumuisha mawaziri wa uchumi Vital Kamerhe, Julien Paluku wa Viwanda na Jean-Lucien Bussa wa Biashara pamoja na kiongozi wa kundi la kisiasa la AAAP, Tony Kanku.
Kamerhe amesema muungano huo mpya utaimarisha mshikamano ndani ya muungano wa vyama tawala.
Upande wa chama cha UDPS chake Rais Tshisekedi umesema hawajaona hasara au shida yoyote kuhusu kuwepo muungano huo ambao wanatumai umeundwa kwa maslahi ya taifa.