1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamati ya wayahudi Marekani miaka 100 leo.

Ramadhan Ali4 Mei 2006

Baraza la wayahudi nchini Marekani (AJC) linaadhimisha leo mwaka wa 100 tangu kuasisiwa. Katika tamasha la kuadhimisha siku hii,Kanzela Angela Merkel wa ujerumani anaezuru Marekani wakati huu,amealikwa kuhutubia pamoja na wageni wengine wa heshima kama mwenyeji wake rais George Bush na Katibu-mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan.

https://p.dw.com/p/CHnP
Picha: picture-alliance / dpa

American Jewish Comittee-Halmashauri ya wayahudi nchini Marekani,iliasisiwa na wayahudi walioihama Ujerumani.lilikua shirika la kwanza la misaada ya kitu nchini Marekani kwa shabaha kwanza kuwasaidia wahamiaji wa kiyahudi pamoja na kuwalinda wayahudi waliokua patarini nchini Russia.Wakati huo huo,halmashauri hii ikijaribu kupalilia ushawishi wake katika jamii ya Marekani.

Mkurugenzi anaehusika na maswali ya kimataifa ya jumuiya hii Rabbi Andrei Baker anatema:

“Naamini ni sehemu ya kilele cha juhudi zetu mnamo karne iliopita kun’gamua kuwa hali za wayahudi nchini Marekani ikishakamana na hatima ya makundi mengine ya wachache .Ndio sababu jumuiya hii ikaweka usoni vita vya kupambana na ubaguzi.”

Kwa kuzidi kupata nguvu za kisiasa ulimwenguni kwa dola la Marekani uliongezeka pia uzito na ushawishi wa jumuiya hii katika maswali ya kilimwengu.Msiba wa kuhilikisha wayahudi-holocaust pamoja na kuundwa kwa dola la Israel kulichangia pia kuzidi kwa umaarufu na nguvu zake.Leo hii,jumuiya hii ina wanachama 150.000 na inahesabika miongoni mwa vikundi vyenye ushawishi mkubwa mno nchini Marekani.

AJC au American Jewish Committee ndio ya jumuiya ya kwanza ya kiyahudi baada ya msiba wa holocaust kuanzisha tena mafungamano na Ujerumani baada ya vita.Tangu miaka ya 1950,jumuiya hii ikiendeleza mabadilishano ya wanafunzi baina ya Ujerumani na jumuiya ya wayahudi nchini Marekani.Miaka 8 iliopita, jumuiya hii ilifungua afisi yake mjini Berlin,kufuatia kuungana tena kwa Ujerumani.

Rabbi Baker anaongeza kusema,

“Mnamo miaka iliopita tumekuwa na ushirikiano mkubwa na serikali ya Ujerumani pamoja na wakfu wake wa kisiasa.Baadhi ya nyakati, ilikua ushirika,wakati mwengine mazungumzo na kuna wakati hata tukigombana.Lakini, mpango wetu wa kubadilishana -hatua muhimu iliochukuliwa miaka 25 iliopita, leo hii ni jambo la kawaida.”

Ushirikiano na serikali ya Ujerumani,ulianzia mutano wa kupiga vita chuki dhidi ya wayahudi-Anti-semitismus Conference chini ya paa la shirika la OSZE mjini Berlin.

Hata chini ya seriali ya sasa ya mungano,ushirikiano huo haukubadilika.Tayari wakati wa ziara yake ya kwanza kabisa nchini Marekani hapo Nov.2005,waziri wa nje wa Ujerumani Walter Steinmeier aliomba ya kuhutubia nafasi ili wakati wa kuadhimisha mwaka 100 wa AJC mjini Berlin hapo Machi,mwaka huu.

Leo ni zamu ya Kanzela Angela Merkel kuseleleza mila hii akiwa mgeni rasmi katika tamasha mjini Washington pamoja na rais Gorge Bush na Katibu mkuu Kofi Annan.