1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yalaani ukiukaji wa Israel katika kuwalinda watoto Gaza

19 Septemba 2024

Kamati ya Umoja wa Mataifa imelaani hivi leo ukiukwaji mkubwa wa Israel wa mkataba wa kulinda haki za watoto, ikisema hatua zake za kijeshi tangu Oktoba 7 zimekuwa janga kwa watoto wa maeneo ya Palestina.

https://p.dw.com/p/4krI1
Hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza
Watoto wa Kipalestina wamekaa kwenye eneo la shambulio la Israel kwenye huko Deir Al-Balah katikati mwa Ukanda wa Gaza, Septemba 5. 2024 Picha: Ramadan Abed/REUTERS

Mapema mwezi huu, ujumbe wa Israel ulijadiliana katika mfululizo wa vikao vya Umoja wa Mataifa na kudai kwamba mkataba huo hauyahusishi maeneo ya Gaza na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu huku wakisisitiza kuwa nchi yao iko tayari kuheshimu sheria ya kimataifa ya kibinadamu. BragiGudbrandsson, makamu mwenyekiti wa kamati hiyo amesema hali ya kutisha, vifo na madhila wanayopitia watoto havijawahi kushuhudiwa katika historia. Mamlaka ya afya ya Palestina imesema zaidi ya watu 41,000 wameuawa huko Gaza na kwamba zaidi ya 11,300 kati yao ni watoto.