Viongozi wa jamii ya Maasai waishio wilaya ya Ngorongoro kaskazini mwa Tanzania, wametoa tamko la kulaani hali ya ukamataji holela wa wananchi unaoendelea. Inadaiwa kwamba tangu Agosti 16 mwaka huu, serikali ya Tanzania kupitia mamlaka za jeshi na polisi imekuwa ikiwakamata wananchi wa eneo hilo ambapo mpaka sasa idadi ya waliokamatwa inapindukia watu 35. Isikilize ripoti ya Veronica Natalis.