1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Kamanda wa zamani wa IRGC achaguliwa spika wa bunge Iran

28 Mei 2024

Wabunge wa Iran wamemchagua tena kamanda wa zamani wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi - IRGC, Mohammad Baqer Qalibaf, kama spika wa bunge.

https://p.dw.com/p/4gNgN
Nchini Iran, kamanda wa zamani wa IRGC achaguliwa spika wa bunge
Nchini Iran, kamanda wa zamani wa IRGC achaguliwa spika wa bungePicha: ran's Presidency/WANA via REUTERS

Televisheni ya taifa imeripoti kuwa wabunge 198 kati ya 287 walipiga kura ya 'ndio' kumchagua Qalibaf kuwa spika wao.

Kiongozi huyo aliwahi kugombea urais mara mbili bila ya mafanikio na kuamua kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais kwa mara ya tatu ili kuepusha kugawanya kura.

Alifufua tena safari yake ya kisiasa kwa kuwania ubunge mnamo mwaka 2020.

Iran imepanga kufanya uchaguzi wa mapema mnamo Juni 28 kufuatia kifo cha Rais Ebrahim Raisi katika ajali ya helikopta na Mohammad Baqer alitajwa na baadhi ya wachambuzi na hata vyombo vya habari kwamba huenda angelijitosa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi hiyo.