1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JUWAYA: UNICEF ina wasiwasi juu ya mabomu

11 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3p

Shirika la watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, limeeleza wasiwasi wake juu ya mabaki ya mabomu ambayo hayajaripuka nchini Lebanon huku wanafunzi wakijiandaa kurudi shuleni wiki ijayo.

Msemaji wa shirika hilo mjini Geneva Uswissi, Michael Bociurkiw, amesema,

´Shirika la UNICEF lina wasiwasi mkubwa sana kwamba hili linabaki kuwa tisho kubwa kwa usalama wa watoto, hususan wanaporudi shuleni na wanapokwenda katika maeneo ya kucheza.´

Afisa huyo wa UNICEF amesema idadi ya mabomu ambayo hayajaripuka ni kati ya laki moja na milioni moja, mengi yao yakipatikana kwenye miti, waya wa seng´eng´e na viwanja vya kuchezea.