SiasaPanama
José Raúl Mulino achaguliwa rais mteule wa Panama
6 Mei 2024Matangazo
Mulino, ambaye ni mshirika wa karibu wa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo aliyeandamwa na kashfa Ricardo Martinelli, ameshinda kwa asilimia 35 ya kura, baada ya asilimia 90 ya kura kuhesabiwa.
Rais huyo mteule anataka kukomesha uhamiaji haramu kupitia msitu wa Darien katika taifa hilo la Amerika ya Kati.
"Nitazungumza na kila mtu, nitamsaidia kila mtu, nitafanya mambo kuwa sawa. Sipendi makabiliano ya aina yoyote," amesema Mulino.
Mulino, ambaye ni waziri wa zamani wa mambo ya nje, usalama na sheria aliteuliwa kuwa mgombea mbadala wa mwanasiasa mrengo wa kulia Ricardo Martinelli, ambaye aliondolewa kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kukutwa na hatia ya utakatishaji fedha na kuhukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 10 jela.