Josep Borrell afanya ziara fupi Kyiv
9 Novemba 2024Matangazo
Hii ni ziara ya kwanza kufanywa na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Umoja huo tangu Donald Trump kushinda uchaguzi wa Marekani.
Ushindi wa kiongozi huyo wa chama cha Republican umeleta wasiwasi nchini Ukraine na Ulaya kwa Ujumla kwamba Trump anaweza kusitisha msaada wa Marekani kwa Kyiv katika vita vyake kupinga uvamizi wa Urusi nchini humo.
Baerbock awasili Kiev kusisitiza mshikamano
Borrell amesema ujumbe uko wazi kabisa kwamba wameiunga mkono Ukraine kuanzia mwanzo na wataendelea kufanya hivyo kwa muda wote.
Wakati wa kampeni zake, Trump alionesha mashaka ya kuendelea kuiunga mkono kijeshi na kifedha Ukraine akisema anaweza kuwa na makubaliano ya haraka ya kusitisha vita kati ya mataifa hayo mawili.