1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG:Polisi waipekua nyumba ya Makamu wa Rais wa zamani Bwana Jacob Zuma.

18 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEk4

Askari polisi wa Afrika Kusini wameivamia nyumba ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo,Jacob Zuma mjini Johannesburg,ambaye aliachishwa kazi na Rais Thabo Mbeki kutokana na kashfa ya rushwa iliyokuwa inakikabili chama tawala cha ANC.

Wakili wa Bwana Zuma,Michael Hulley,amesema alizungumza na kiongozi huyo wa zamani leo asubuhi na amemthibitishia kuwa nyumba yake ilipekuliwa.

Polisi hawakuweza kupatikana kuzungumzia lolote juu ya upekuzi huo ulioendeshwa mapema leo asubuhi,ambao magazeti ya Afrika Kusini yamedai kuwa hata ofisi ya mshauri wa zamani wa masuala ya fedha wa Bwana Zuma,Schabir Shaik iliyopo mjini Durban,nayo ilivamiwa na polisi.Bwana Schabir alipatikana na hatia ya kuhusika na vitendo vya rushwa mwezi Juni,kesi ambayo iliibua mashtaka pia kwa Makamu wa Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini.

Hata hivyo askari polisi hao walizuiwa na walinzi wa Bwana Zuma kuendelea na upekuzi,hadi hapo Bwana Zuma mwenyewe awepo.Haikujulikana Bwana Zuma alikuwa wapi wakati huo.