1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jimbo la Kivu Kusini lahitaji dola mil. 56 kujijenga upya

31 Mei 2024

Tathmini kuhusu Jimbo la Kivu Kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeonesha kwamba eneo hilo linahitaji angalau dola milioni 56 kuweza kukabiliana na matatizo ya kiusalama na miundombinu.

https://p.dw.com/p/4gVao
MONUSCO nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa katika jimbo la Kivu Kusini umesitisha shughuli zake na kuondoka kwenye eneo hilo.Picha: AA/picture alliance

Kiasi hicho kinahitajika ili jimbo hilo liweze kustawi baada ya Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa, MONUSCO, kuondoka.

Tathmini hiyo imetangazwa baada ziara ya Ujumbe wa Wafadhili wa Kongo unaoongozwa na Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo, Bruno Lemarqui, katika jimbo hilo.

Ujumbe huo pia umeikumbusha serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwamba kwamba inawajibika kuhakikisha usalama wa raia wake pamoja na shughuli nyingine muhimu zilizokuwa zikifanywa MONUSCO

Ujumbe huo umeahidi kufanikisha hatua zinazofuata za kuondoka kikosi cha Umoja wa Mataifa MONUSCO kutoka kwenye majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri.