1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Warepublican wa Iowa, Marekani kuchagua mgombea urais 2024

15 Januari 2024

Wajumbe wa chama Republican katika jimbo la Iowa nchini Marekani watapiga kura leo wakifungua pazia la kura za mchujo za kumteua mgombea wa urais wa chama hicho katika uchaguzi wa baadaye mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4bEey
Marekani | Donald Trump
Donald Trump anaongoza kura za maoni jimbo la Iowa.Picha: Kamil Krzaczynski/AFP/Getty Images

Zoezi hilo la leo litakuwa kipimo cha kwanza kwa rais wa zamani Donald Trump anayewania kuteuliwa kuwa mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi wa rais wa mwezi Novemba. Anachuana na wagombea wengine wawili Nikki Haley na Ron DeSantis.

Trump anaongoza kura za maoni ya umma na anatazamiwa kushinda kura hiyo ya kwanza ya mchujo katika jimbo hilo la magharibi mwa Marekani.

Kuna wasiwasi hali mbaya ya hewa iliyosababishwa na kimbunga cha theluji inaweza kutatiza zoezi la upigaji kura huko Iowa. Hata hivyo Trump amewatolea mwito wapiga kura wa Republican kuikabili baridi na kujitokeza kwa wingi kumchagua.