Jeshi limewazuwia wakimbizi 1,200 wa Syria kuingia Lebanon
7 Septemba 2023Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati mapema leo alielezea wasiwasi wake kuhusu wimbi jipya wa wakimbizi wanaovuka mipaka kwa kupitia njia zilizo kinyume na sheria.
Ameongeza kuwa, jeshi la nchi hiyo na askari polisi kwa pamoja wanalishughulikia suala hilo. Nchi hiyo ilitangaza Agosti 13 kuwa iliwarejesha kwao raia 700 wa Syria waliokuwa wakijaribu kuingia nchini humo kinyume cha utaratibu.
Soma zaidi: Lebanon yaanza kuwarejesha wakimbizi wa Syria
Mamilioni ya wa Syria wamekimbilia mataifa mengine tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipoanza mwaka 2011 baada ya serikali kuzuia maandamano dhidi ya serikali ya Rais Bashar al-Asad. Wengi wao wamevuka mpaka kuingia Lebanon nchi ambayo kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, inahifadhi idadi kubwa ya wakimbizi.