1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yasema Urusi inajiimarisha kijeshi dhidi ya NATO

23 Julai 2024

Inspekta mkuu wa majeshi ya Ujerumani Carsten Breuer amesema anaona hatari inayoongezeka katika kujijenga kijeshi kwa Urusi kwa uelekeo wa mipaka ya mataifa Magharibi.

https://p.dw.com/p/4ideS
Berlin
Inspekta mkuu wa majeshi ya Ujerumani Carsten Breuer Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Akizungumza na gazeti la Kijerumani "Sächsische Zeitung" amesema katika kipindi cha miaka mitano hadi minane jeshi la Urusi litakuwa limejitosheleza kwa vifaa na askari, hatua ambayo inaweza kuipa uwezo wa kuyashambulia mataifa ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO.

Mkuu huyo alionekana akiunuku uchambuzi wake mwenyewe, ripoti za kijasusi na taarifa kutoka vikosi vya washirika, pamoja na matamshi ya Rais wa Urusi Vladimir Putin, kama msingi wa tathmini hizo.

 

Jeshi la Urusi limeongeza idadi ya vifaru kwa idadi ya 1,000 hadi 1,500. Lakini wanachama wakubwa wa NATO wa Ulaya kwa pamoja, yana nusu tu ya idadi hiyo katika orodha yao.