1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Myanmar lakiri kuwatesa wafungwa

Deo Kaji Makomba
13 Mei 2020

Jeshi la Myanmar limekiri wazi wazi kwamba vikosi vyake viliwafanyia vitendo vya unyanyasaji ambavyo ni kinyume na haki za binadamu wafungwa katika jimbo la Rakhine.

https://p.dw.com/p/3cAwV
Ungarn Suu Kyi Archiv
Picha: Getty Images/A. Kisbenedek

Kitendo hicho ambacho ni nadra kwa jeshi hilo kukiri kutokana na makosa ya utumiaji nguvu na kutokujali mara nyingi. 

Video hiyo, ambayo ilianza kuonekana katika mitandao ya kijamii tangu jumapili iliyopita, ilionyesha wanaume waliokuwa vifua wazi wakipiga ngumi na mateke vichwa vya wafungwa waliofungwa mikono na kufungwa macho kwa nguo.

Wafungwa watano walikamatwa kwa tuhuma za kuwa wapiganaji katika kikosi cha Arakan walihamishiwa kwenye mji mkuu wa jimbo la Rakhine Sittwe kwa boti hapo April 21 wakati tukio hilo lilipotokea, hii ni kwa mujibu tovuti ya mkuu wa jeshi.

Majeshi ya Myanmar yamenasa katika vita vikali vya umwagaji damu na ukatili na waasi, ambao wanapigania uhuru zaidi wa kujitawala kwa jamii ya Budha ya jimbo la Rakhine.

Baadhi ya maafisa usalama wa jeshi waliwahoji wafungwa katika njia iliyo kinyume cha sheria na hatua zitachukuliwa kwa wale wote walio husika, taarifa ya jeshi hilo ilieleza bila kutoa ufafanuzi ni adhabu gani watakabiliana nayo wale waliofanya vitendo hivyo.

Video hiyo ya nadra kuonekana wakati wa operesheni za jeshi lililoshutumiwa kila mara kwa unyayasaji wa dhuluma ya kiubinadamu ilisambazwa na kuleta maoni mseto kati ya watu wanaopinga vitendo hivyo na wale wanaowatetea wanajeshi.

Familia za wanaume waliokamatwa zimekanusha kuwa na mahusiano na  kikundi cha AA. "alikuwa akifanya kazi katika duka la mchele. Hakujua chochote kuhusiana na AA," Ni Ni, mama wa mfungwa mwenye umri wa miaka 24  Nyi Nyi Aung aliliambia Shirika la habari la AFP kwa njia ya simu.

Video hiyo inamuonesha afisa aliyemuhoji Nyi Nyi akikisukuma kichwa chake kutumia nywele huku akimpiga ngumi usoni, kabla mlinzi mwingine kumpiga kichwani.
 
Watu wengi waliuwawa na mamia kujeruhiwa na baadhi ya watu 150, 000 wameyakimbia makazi yao tangu mapigano yalipoibuka mwezi January mwaka jana.

Yanghee Lee ambaye anahusika na masuala ya haki za binadamu kutoka  Shirika la Umoja wa mataifa, mwezi uliopita alilionya jeshi la Myanmar na kuongeza kuwa jeshi hilo linapaswa kuchunguzwa kutokana na kuhusika katika uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika mzozo huo.

Lee alilishtumu jeshi kwa  kupotea, kuwatesa na kuwauwa watuhumiwa kadhaa wa kikundi cha AA, na pia kuzuia misaada na kuwazuia raia waliojeruhiwa kufika hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Myanmar inakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kimbari katika mahakama kuu ya Umoja wa mataifa kesi iliyoletwa baada ya Waislamu wapatao 740,000 wa Rohingya kukimbilia nchini Bangladesh katika shambulio la kijeshi la umwagaji damu la 2017 huko Rakhine.

Amnesty International yataka wanajeshi Myanmar wafikishwe ICC

Myanmar - Hinduistische Dorfbewohner massakriert in Rakhine
Picha: Getty Images/AFP
Myanmar Rohingya-Flüchtlinge aus Bangladesch | Polizei & Journalisten Thet Kae Pyin-Camp
Picha: Getty Images/AFP/P. Hein Kyaw

Mashirika: AFP