1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel latoa amri ya watu kuuhama mji wa Gaza

10 Julai 2024

Jeshi la Israel leo limewaamuru maelfu ya waakazi wa mji mkubwa zaidi kwenye Ukanda wa Gaza kuondoka katika wakati linazidisha mashambulizi yake kwenye eneo hilo la Wapalestina.

https://p.dw.com/p/4i7ax
Wakaazi gaza wakitafuta manusura kwenye kifusi.
Wakaazi wa Gaza wakitafuta manusura katika kifusi baada ya shambulio la IsraelPicha: EYAD BABA/AFP via Getty Images

Kupitia vipeperushi vilivyodondoshwa kwenye mji wa Gaza, jeshi la Israel limemtaka "kila mmoja aliye ndani ya mji wa Gaza" kuondoka kuelekea kwenye maeneo salama kusini mwa Ukanda huo. 

Ujumbe kwenye vipeperushi hivyo umeonya kwamba eneo lote la mjini litabakia uwanja hatari wa vita wakati Israel inapambana kutokomeza kile imekitaja kuwa ngome za wapiganaji wa Hamas. 

Soma pia:Israel yazidisha mashambulizi dhidi ya Gaza

Duru zinasema waakazi wametolewa mwito wa kutumia njia mbili salama kwenda kwenye makaazi ya muda yaliyotengwa ya Deir Al-Balah na Al-Zawiya. 

Amri ya watu kuhama imetolewa katikati mwa hujuma zinazoongeza kwenye Ukanda wa Gaza ambapo Israel inatumia ndege za kivita na vifaru kuyambulia maeneo tofauti ya ukanda huo.