1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Jeshi la Israel latanua operesheni zake hadi kusini mwa Gaza

4 Desemba 2023

Jeshi la Israel limesema limetanua operesheni yake ya ardhini dhidi ya kundi la Hamas katika kila sehemu ya Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4ZjWo
Nahostkonflikt | Rafah
Wanawake wa Palestine wakiomboleza kifo cha mtoto aliyeuawa huko Rafah katika Ukanda wa Gaza: 01.12.2023Picha: AFP

Baada ya kuelekeza operesheni hizo katika eneo la kaskazini katika wiki za hivi karibuni, Israel imeanzisha pia mashambulizi ya anga kusini mwa Gaza, walipokimbilia idadi kubwa ya watu.

Awali, Msemaji wa jeshi wa jeshi la Israel Daniel Hagari amethibitisha kuwa vikosi vyao vimekuwa vikipiga hatua kuelekea kusini. Mashuhuda wameliambia shirika la habari la Ujerumani DPA kuwa wanajeshi wa Israel wameingia eneo la mashariki mwa mji wa Khan Yunis  kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF) limesema linashuhudia "maafa makubwa ya watoto." Msemaji wa UNICEF James Elder aliyekuwa kusini mwa Gaza ameeleza kwamba eneo hilo kwa sasa linakabiliwa na "mashambulizi mabaya zaidi katika vita hivyo."