1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel lashutumiwa kumuua kijana wa kipalestina

27 Aprili 2022

Vikosi vya jeshi la Israel vimempiga risasi na kumuua kijana mmoja wa kipalestina na kuwajeruhi wengine watatu katika makabiliano yaliyozuka kwenye la Ukingo wa Magharibi linalokaliwa kwa mabavu na Israel.

https://p.dw.com/p/4AV6V
WS | Israel Palästina Zusammenstöße in der Westbank
Picha: Jaafar Ashtiyeh/Getty Images/AFP

Taarifa ya wizara ya afya ya mamlaka ya ndani ya Palestina imesema kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 alikufa kutokana na majeraha ya risasi ya kichwa na wenzake watatu pia wamejeruhiwa baada ya kufyetuliwa risasi za moto.

 Kwa upande wake Jeshi la Israeli limesema mkasa huo umetokea baada ya wapalestina kuwarushia mawe na vilipuzi wanajeshi wa Israel waliokuwa wakifanya  operesheni maalamu kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi.

soma zaidi: Mapigano mapya yaripotiwa mjini Jerusalem

Kisa hicho cha leo kinajiri siku chache baada ya kuzuka machafuko kati ya Israel na wapalestina yaliyoshuhudia polisi ya Israeli ikitumia nguvu kuwakabili wapalestina katika eneo takatifu kwa waislamu la msikiti wa Al-Aqsa mjini Jerusalem.

Chanzo: ap