Jeshi la Israel lamuua kamanda meingine wa Hezbollah
30 Oktoba 2024Israel leo imesema imemuua naibu wa kamanda mkuu wa kikosi maalumu cha kundi la Hezbollah cha Radwan Force, Mustafa Ahmad Shahadi, katika shambulizi lililofanywa eneo la Nabatieh kusini mwa Lebanon.
Taarifa ya jeshi la Israel imesema katika shambulizi lililofanywa kwa kuongozwa na taarifa za kijasusi, jeshi la anga la Israel limemshambulia na kumuua kamanda huyo.
Imongeza kwamba Shahadi awali alikuwa akiendesha operesheni za kikosi cha Radwan nchini Syria na kusimamia mashambulizi ya kigaidi kusini mwa Lebanon.
Wakati haya yakiarifiwa, kiongozi mpya wa kundi la Hezbollah, Naim Qassem, amesema ataendeleza mkakati wa vita uliowekwa na mtangulizi wake Hassan Nasrallah aliyeuwawa na vikosi vya Israel mwezi uliopita wakati vita kamili kati ya Israel na Hezbollah vilipozuka.