1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel laamuru watu waondoke kaskazini mwa Gaza

7 Agosti 2024

Jeshi la Israel limetoa agizo lingine kuwataka watu waondoke kwenye maeneo ya kaskazini mwa Ukanda wa Gaza ambayo yalikuwa ya kwanza kushambuliwa baada ya vita na Hamas kuzuka mnamo mwezi Oktoba mwaka jana.

https://p.dw.com/p/4jDL7
Hali ya Ukanda wa Gaza
Hali ya Ukanda wa Gaza.Picha: Abdel Kareem Hana/AP/dpa/picture alliance

Jeshi la Israel limetoa amri hiyo baada ya kufanyika mashambulio ya makombora kuilenga nchi hiyo.

Msemaji wa jeshi ametangaza amri hiyo inayozihusu wilaya kadhaa za miji mikubwa miwili ya Beit Hanoun and Beit Lahiya iliyoharibiwa na vifaru vya Israel vilipoingia mwanzoni mwa vita.

Kwa mujibu wa wizara ya afya kwenye Ukanda wa Gaza, watu 24 wameuawa katika muda wa saa 24 zilizopita.

Aidha, wizara hiyo imesema tangu kuanza kwa vita, Wapalestina zaidi ya elfu 39 wameuawa na wengine 91,645 wamejeruhiwa.