1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, Ulaya itaiwekea vikwazo Belarus?

19 Agosti 2020

Mgogoro wa kisiasa nchini Belarus bado unaendelea kutokota.Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanaokutaka kwenye mkutano wa dharura wa kilele wanatarajiwa kuidhinisha vikwazo dhidi ya maafisa wa nchi hiyo ya Mashariki mwa Ulaya.

https://p.dw.com/p/3hBwL
EU Virtueller Gipfel Belarus Belgien Charles Michel
Picha: Reuters/O. Hoslet

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana kuzungumza kwa njia ya video kwenye kikao hicho cha dharura na kinachotarajiwa tayari kimeshadokezwa. Maafisa wa Belarus wanaolaumiwa katika mizengwe ya uchaguzi na wizi wa kura ndio watakaowekewa vikwazo.

Ingawa pia viongozi hao wa Umoja wa Ulaya wameonesha dalili kwamba hawako tayari kuchukua hatua ambazo huenda zinaweza kuonekana kama juhudi za kuiondowa nchi hiyo katika mwelekeo wake wa kuigemea zaidi Urusi. Rais Alexander Lukashenko anakabiliwa na maandamano makubwa mitaani tangu maafisa wa tume ya uchaguzi walipomtangaza mshindi Agosti tisa katika uchaguzi ambao wapinzani wake wanasema udanganyifu ulifanyika.

Wapinzani wa Belarus wanaishi katika mazingira magumu

Vilnius Litauen Protest Belarus Botschaft
Waandamanaji karibu na ubalozi wa Belarus LithuaniaPicha: Imago Images/D. Mataitis

Mamlaka nchini humo zimewaandama wapinzani huku naelfu ya watu wakikamatwa nchini humo. Huu ni mgogoro mkubwa katika nchi hiyo iliyokuwa ya kisovieti tangu ziliposhuhudiwa harakati zilizopata umaarufu mkubwa katika eneo hilo zilizomuondowa madarakani kiongozi wa Ukraine aliyekuwa akiegemea upande wa Urusi miaka sita iliyopita. Harakati ambazo zililifanya jeshi la Urusi kuingilia kati katika nchi hiyo ya Ukraine na kusababisha mgogoro wa umwagikaji mkubwa wa damu unaoendelea hadi sasa barani Ulaya.

Mwenyekiti wa mkutano huo wa kilele wa Umoja wa Ulaya Charles Michel amehimiza amani kwa kuandika ujumbe kupitia mtandao wa Twita akisema,vurugu zinabidi zisitishwe na mazungumzo ya amani yanayojumuisha pande zote yaanzishwe.

Matarajio ya vikwazo vya kiuchumi

EU Virtueller Gipfel Belarus Belgien Charles Michel
Mjadala kuhusu Belarus unafanyika kwa njia ya videoPicha: Reuters/O. Hoslet

Lakini pia kwenye kikao hicho viongozi wa Umoja wa Ukaya wanatarajiwa kuidhinisha vikwazo vya kiuchumi kwa maafisa wa Belarus wanaotwishwa dhamana ya wizi wa kura katika uchaguzi huo na kuwaandama waandamanaji.

Svitlana Tsikhanouskaya aliyekimbilia nchi jirani ya Lithuania, mwanamama mwenye umri wa miaka 37 ndiye mpinzani mkubwa aliyepambana na Lukashenko kwenye uchaguzi huu baada ya wapinzani wengine wenye umaarufu mkubwa kutiwa jela au kuzuiwa kugombea na amewatolea mwito viongozi wa Umoja wa Ulaya kuupinga ushindi wa Lukashenko.

Lakini viongozi wa Umoja wa Ulaya wameshasema wazi kabisa kwamba hawadhamirii sana kuchukuwa hatua kubwa za kuunga mkono upinzani kitu ambacho kikifanyika kuna uwezekano kikachochea Urusi kuingilia kati. Kamishna wa viwanda katika Umoja wa Ukaya Thierry Breton anasema Belarus haiko upande wa Umoja wa Ulaya, ukiilinganisha na nchi zinazoegemea upande wa Magharibi kama Ukraine na Georgia ambazo zote zinalengwa na operesheni za kijeshi za Urusi.

Soma zaidi: Upinzani: EU usiutambue uchaguzi wa Belarus

Ameongeza kusema Belarus inamafungamano makubwa zaidi na Urusi na wananchi wake wengi wanapendelea zaidi mahusiano na Urusi.Lukashenko ameshaitawala Belarus kwa miaka 26.

Chanzo: RTR/AFP