Chama tawala nchini Tanzania, CCM kimemteua Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu ujao. Hata hivyo kuna sauti zinazolalamikia kukiukwa kwa utaratibu wa chama kutokana na mchakato huo kuonekana kufanyika mapema kuliko kawaida. Mohammed Khelef amezungumza na Katibu mwenezi na Itikadi taifa Amos Makalla kuhusu udharura huo. Sikiliza.