Viongozi wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika wamefikia maazimio kadhaa kutokana na mkutano wao mjini Addis Ababa mwishoni mwa juma na mojawapo ni kuandaa mkutano wa maridhiano ya kitaifa kwa ajili ya Libya. Je, ni kwa umbali gani Umoja huo unaweza kufanikiwa katika maazimio ya mkutano huo? Sikiliza mahojiano kati ya Saumu Mwasimba na mchambuzi wa kisiasa Ali Mali kutoka visiwani Comoros.