Waziri wa afya wa Tanzania Dorothy Gwajima alitoa amri ya kukamatwa kwa mbunge Josephat Gwajima kwa kile kinachodaiwa kuwa upotoshaji juu ya chanjo ya virusi vya Corona. Lakini Gwajima anaweza kukamatwa kwa kosa hilo? Slyvia Mwehozi amezungumza na Dr. Edward Hosea, rais wa chama cha wanasheria Tanganyika TLS.