1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Japan yashuhudia viwango vya juu vya joto

Sylvia Mwehozi
1 Septemba 2023

Nchi kadhaa ulimwenguni zimeendelea kuripoti hali ya joto na baridi kali.

https://p.dw.com/p/4VrBj
Hitzewelle in Japan
Picha: Issei Kato/REUTERS

Mamlaka ya hali ya hewa ya Japan imesema leo kwamba msimu wa majira ya kiangazi ulikuwa wa joto kali zaidi kwa mwaka huu na kuvunja rekodi katika kipindi cha miaka 125 iliyopita.

Kulingana na mamlaka hiyo ya hali ya hewa, kiwango cha wastani cha joto kilikuwa cha juu zaidi katika maeneo ya kaskazini, mashariki na magharibi mwa nchi.

India, nchi yenye idadi kubwa ya watu duniani, ilishuhudia hali ya  joto kali na ukavu kwa mwezi Agosti na kuvunja rekodi zaidi ya karne moja iliyopita. Wakati nchi za kaskazini mwa dunia zikiripoti rekodi za joto la kiangazi, nchini Australia, kumeripotiwa msimu wa baridi kali zaidi katika rekodi za nchi hiyo.