1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Japan yalalamikia 'harakati za jeshi' China

10 Oktoba 2024

Waziri mpya wa mambo ya kigeni wa Japan amewasilisha rasmi kwa mwenzake wa China, malalamiko juu ya kuongezeka kwa harakati za kijeshi za Beijing, zikiwemo zile zinazongilia anga la Tokyo.

https://p.dw.com/p/4lbWh
Wang Yi
Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi.Picha: Heather Khalifa/Pool(REUTERS

Takeshi Iwaya aliiambia Wang Yi kwa njia ya simu hapo jana kwamba nchi yake ilikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya hali inavyoendelea kwenye Bahari ya China Mashariki, likiwemo tukio la mwezi Agosti, ambapo ndege ya kijeshi ya China na safari ya meli ya kijeshi ya mwezi Septemba.

Soma zaidi: China yafanya luteka karibu na Bahari ya China Kusini

Waziri huyo mpya wa mambo ya nje wa Japan ametaka apatiwe ufafanuzi rasmi  kutoka kwa mwenzake wa China.

Taarifa kutoka Beijing imesema kwenye mazungumzo hayo, Wang alimuelezea mwenzake wa Japan kwamba Beijing inatazamia kufanya naye kazi kwa moyo mpya wa ushirikiano na maendelea ya pande zote mbili.