1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Japan, Uingereza na Italia kuunda ndege ya kisasa ya kivita

9 Desemba 2022

Uingereza, Italia na Japan zimefahamisha leo kuwa zitaunda kwa pamoja ndege ya kivita katika mradi ambao Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amesema utasaidia kuhakikisha usalama wa taifa na kulinda maelfu ya ajira.

https://p.dw.com/p/4KjrF
Vietnam als Regionalmacht/Anlass Waffenmesse 2022 in Hanoi
Picha: Nhac Nguyen/AFP

Mataifa hayo matatu yalibainisha matarajio ya ushirikiano na washirika wa Ulaya na Marekani, ambao wanaunda ndege zao za "kisasa za kivita", wakiahidi kudumisha "ushirikiano" kati ya washirika wote dhidi ya vitisho kutoka kwa mataifa kama China na Urusi.

Mpango huo mpya wa vifaa vya angani unatazamiwa kutengeza ndege za kwanza ifikapo mwaka 2035, kwa kujumuisha utafiti wenye gharama kubwa wa mataifa hayo matatu katika teknolojia mpya ya vita vya angani.

Hata hivyo maafisa wa Tokyo wamesisitiza kwamba Japan haitaupa kisogo muungano wake wa karibu wa kijeshi na Marekani.