James Mbatia akaidi kuwekwa kando ya nafasi yake
26 Mei 2022Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya NCCR Mageuzi na Mwenyekiti wa azimio la kumsimamisha Mbatia, Joseph Selasini, ametaja sababu za kumsimamisha uongozi Mbatia na wenzake kuwa ni kwa sababu Mbatia alitumiwa na CCM wakati wa uongozi wa Hayati John Magufuli.
Itakumbukwa kwamba chama cha NCCR kilipeleka maamuzi ya kuwasimamisha shughuli za kisiacha ndani ya chama hicho mwenyekiti wake pamoja na sekretarieti yake, ikiwashutumu kwenda kinyume na katiba ya chama chao ikiwa ni pamoja na kuwagombanisha wananchama kadhalika kutumiwa kisiasa.
Soma pia→Rais Samia: Tanzania haiwezi kujengwa na chama kimoja
''Mimi ni mwenyekiti halali''
Hata hivyo katika mkutano wake na waandishi wa habari James Mbatia, aliyesimamishwa kuwa Mwenyekiti, wa chama hicho cha upinzani ambacho kilijizolea umaarufu zaidi katika miaka ya tisini , amepinga uamuzi huo ambao uliridhiwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini, akisema kwa mujibu wa katiba ya chama chake yeye bado ni mwenyekiti halali wa chama hicho cha upinzani kwani kikao kilichokaa kumsimamisha ni batili.
''Kwa mujibu wa sheria,kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mimi ni mwenyekiti halali wa NCCR-Mageuzi.''
Uamuzi huo umetajwa kuzusha mgogoro ndani ya chama hicho huku wale wanaopinga azimio hilo ankiishutumu hadharani ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini kuwa ni chanzo cha migogoro mingi ndani ya vyama vya upinzani.Katibu wa uenezi wa chama hicho, Edward Simbeye, anasema kuna haja ya kuwa na jicho la ziiada katika ofisi ya msajili.
Hoja hii inaungwa mkono na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa. Deus Kibamba amesema hata hivyo nilimtafuta Naibu Msajili wa Vyama vya siasa, Cyst Nyahoza, kwa ajili ya kujibu hoja hiyo badala yake alisema yupo kwenye mkutano.Hadi tunakwenda mitamboni, hatukuweza kupata wasaa wa kuzungumza na Nyahoza.