1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jakarta:Kesi ya vikatuni vya kudhihaki uislamu.

21 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG5J

Muandishi wa habari wa Indonesia aliyekuwa akichunguzwa kuhusu kuchapisha katuni yenye kumdhihaki mtume Mohammad mwaka uliopita huenda akakabiliwa na mashtaka.

Muendesha mashtaka amedai kuwa, Teguh Santosa mhariri mkuu wa gazeti la Rakyat Merdeka siku ya Jumatano itakuwa ndio siku ya mwisho wa kesi yake ya kufuru.

Ikiwa kesi hiyo itafikishwa mahakamani na majaji kumuona Santosa ana hatia ya kuidhihaki dini, atakabiliwa na hukumu ya kifungo cha miaka mitano jela.

Santosa aliachiliwa mapema leo kufuatia malalamiko kutoka kwea waandishi wa habari na baadhi ya maafisa wa serikali, na baada ya upande wa utetezi kumaliza kujaza fomu ya malalamiko.

Indonesia ni moja kati ya nchi maarufu hapa duniani zenye waislamu wengi.