JamiiBrazil
Jaji wa Brazil aamuru kufungwa kwa mtandao wa X nchini humo
31 Agosti 2024Matangazo
Uamuzi huo unajiri baada ya X kushindwa kutii amri ya kumteua mwakilishi mpya wa kampuni hiyo. Sheria ya Brazili inazitaka kampuni zote zinazomiliki mitandao ya kijamii kuwa na mwakilishi wa kisheria katika nchi hiyo ya Amerika Kusini.
Mapema mwezi huu, mtandao wa X ulimuondoa mwakilishi wake nchini Brazil baada ya Jaji wa Mahakama ya Juu ya Brazil Alexandre de Moraes kutishia kumkamata.
Soma pia: Elon Musk kushitakiwa Brazil
Kwa wiki kadhaa sasa, Jaji Moraes na mmiliki wa X Elon Musk wamekuwa kwenye mvutano juu ya masuala ya uhuru wa kujieleza, akaunti zenye itikali kali za mrengo wa kulia pamoja na habari potofu.