Jacob Zuma na ANC
21 Desemba 2007Kati ya wiki hii, Jacob Zuma alimuangusha kitini rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na kushika wadhifa wa urais wa chama-tawala cha ANC-wadhifa unaomfungulia mlango kuja kuwa rais wa nchi hiyo.Haukupita lakini muda imedhihirika kwamba n jia ya kuelekea Ikulu-Pretoria- kwa Zuma ina miba na si rahisi hivyo.Haukupita muda pia kumebainika badiliko la mtindo baina ya rais Mbeki na Bw.Zuma,mwenyekiti mpya wa chama.Zuma anazungumza kwa ubashasha mkubwa tangu na waandishi habari hata wajumbe wenzake wa chama ,kinyume kabisa na tabia ya mtangulizi wake - Thabo Mbeki, aliekua akijitenga nao.
Nani huyu mwenyekiti mpya wa ANC-Jacob Zuma ?
Kwani, watu wengi wameonesha kufadhahika na kuduwaa juu ya kigogo hiki kinachojiwinda kuja kushika usukani war ais Mbeki hapo 2009.Swali hili lachomoza kutokana na washtaki wa serikali kutangaza wana ushahidi wa kutosha wa kumshtaki Bw.Zuma kula rushua.
Mchambuzi mmoja wa siasa za Afrika kusini Adam Habib wa Baraza la taftishi za sayansi ya mwanadamu alisema,
„Badiliko kubwa ni kuwa hatutakua tena mwenyekiti wa chama ,bali tutakuwa na mtu atakaecheza pamoja nasi ngoma jukwaani .
Akaongeza lakini, „Situmai patakuwapo badiliko kubwa la sera .Ikiwa kutafanyika mabadiliko yoyote basi ni katika sekta ambazo hazitazusha mtaharuk au wasi wasi katika masoko ya dunia.“
Badiliko hilo ni pamoja na maswali-pacha ya kuupiga vita uhalifu na maradhi ya UKIMWI.Ni mada hizo 2 alizozipigia mno upatu Bw.zuma katika katika hotuba yake ya ufunguzi akiwa mwenyekiti mpya wa chama cha ANC.
Zuma alitumia hotuba yake jana mkutanoni kuitisha pawepo umoja chamani akimpongeza Mbeki na kuondosha hofu zas kuwapo mpapurano kati ya mashina 2 ya madaraka-rais na chama. Shina la serikali liliopo Pretoria na Makao makuu ya chama mjini Johannesberg.
Wakati Bw.Thabo Mbeki akiwakwepa waandishi habari kwa kadiri awezavyo, Zuma akionesha hana taabu nao huku akifanya nao maskhara katika mkutano na waandishi habari.
Lakini wakati amempiku mno rais Mbeki kwa ubashasha na ucheshi, Zuma ameliacha taifa hili linajiuliza litarajie nini kutoka kwake siku zijazo ? jibu lake Bw.Zuma ni hili: Maamuzi kuhusu sera za ANC hukatwa na mkutano wa chama na sio na mtu mmoja binafsi.“
Kwa muujibu wa Bibi Susan Booysen ,mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Wits Uiniversity- urais wa Bw.Zuma ungali umebaki kuwa kitu kisichofahamika.Kwani, ameiacha nchi, asema Bibi Booysen katikka hali ya wasi wasi kutokuja kitafuata nini.
Mhadhiri huyo adai kuwa yungali akisaka kitu madhubuti cha kutegemea katika jukwaa la kisiasa hakioni kujua Bw.zuma anatetea nini ana simama wapi ?
Bw.Jacob zuma na wafuasi wake walikumba viti vingi katika uchaguzi wa chama huko Polokwane.Walinyakua nyadhifa 6 za usoni kabisa za chama-tawala cha ANC na kuwatimua mawaziri 8 wa rais Mbeki kutoka halmashauri kuu tendaji ya chama-tawala.Pale matokeo yalipotangazwa,Mbeki aliondoka jukwaa akiona haya macho chini.Zao la siasa zake za kinguvunguvu na kusahau alikotoka.