Israel yatakiwa kutekeleza hatua za kusitisha mapigano Gaza
13 Novemba 2024Blinken amesema Israel imechukuwa hatua nyingi kushughulikia mzozo wa kibinadamu kabla ya kukamilika kwa muda uliowekwa na utawala wa Rais wa Marekani anayeondoka Joe Biden, lakini mengi yanahitajika kufanywa.
Blinken asema "sasa ni wakati" wa kuvimaliza vita vya Gaza
Katika mkutano na waandishi wa habari leo wakati wa ziara yake mjini Brussels nchini Ubelgiji, Blinken amesema nia ilikuwa kuihimiza kwa dharura Israel kuchukua hatua zinazohitajika kushughulikia hali mbaya ya kibinadamu katika eneo hilo la Gaza inayowakabili watoto, wanawake na wanaume.
Masuala yanayopaswa kutekelezwa na Israel
Kusitishwa kwa mipagano kwa muda ni moja kati ya masuala hayo.
Blinken ameongeza kuwa masuala hayo mengine mawili ni kuruhusu malori ya kibiashara kuingia katika eneo hilo la Kipalestina na kubatilisha maagizo ya kuhama kwa wakazi ili watu waweze kurejea katika eneo hilo baada ya Israel kukamilisha operesheni zake za kijeshi.
Marekani yasema Israel kuongeza kivuko kuingiza misaada Gaza
Mjumbe huyo mkuu wa Marekani pia amesema mbali na kumaliza vita hivyo, ambavyo waamini sasa ndio wakati muafaka wa kufanya hivyo, wanapaswa kuona kuwa hatua hizo za kibinadamu zinatekelezwa kikamilifu.
Shambulizi la Israel lawauwa Wapalestina 22, Gaza
Shambulizi la kijeshi la Israel limewauwa Wapalestina 22 kote katika ukanda wa Gaza leo huku wanajeshi hao wakizidi kuvamia mji wa Beit Hanoun katika eneo la kaskazini na kuwalazimu wakazi waliobaki kuondoka .
Wakazi wa eneo hilo wanasema vikosi vya Israel vilizingira eneo linalohifadhi familia zilizopoteza makazi yao na idadi yawatu iliyobaki inayokadiriwa kuwa katika maelfu na kuwaamuru kuelekea katika eneo la kusini kupitia kituo cha ukaguzi kinachotenganisha miji miwili na kambi ya wakimbizi katika eneo la kaskazini kutoka Gaza City.
Netanyahu: Hakuna eneo tusiloweza kulilenga Mashariki ya Kati
Wakazi pamoja na madaktari wa Palestina wanasema wanaume walizuiliwa kuhojiwa huku wanawake na watoto wakiruhusiwa kuelekea Mji wa Gaza.
Makubaliano ndio njia sahihi ya kuachiwa huru kwa mateka wa Israel
Kundi moja la Israel linaloshinikiza kuachiwa huru kwa mateka wanoshikiliwa katika ukanda wa Gazalinalojulikana kama Mateka na Familia Zilizopotea, limesema leo kwamba wapendwa wao hawana tena muda kufuatia hatua ya kundi la wanamgambo la Hamas ya kuchapisha video ya mateka mmoja.
Israel yaendeleza mashambulizi Gaza na lebanon
Kundi hilo la Israel, limesema makubaliano ya kuachiwa huru kwa mateka hao ndio njia ya pekee ya kuhakikisha wanarudi nchini mwao.